编辑: 黎文定 2016-09-04

26 SURA YA NANE: Mtume kuchaguliwa mfalme wa Madina - vita vya Mtume kisa cha Uhud

32 SURA YA TISA: Kisa cha Hunain na nguvu za Utume - hotuba ya mwisho ya Mtume

37 SURA YA KUMI: Tabia ya Mtume - Mafundisho ya Mtume

42 v vi RAMANI YA BARA ARABU SURA YA KWANZA Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na Ukoo wake Kama miaka elfu moja na mia nne iliyopita, siku ya tarehe

20 Aprili

571 A.D., mtoto alizaliwa Makka, mji katika Bara Arabu kiasi cha maili arobaini kutoka kwenye ukingo wa bahari ya Red Sea (Bahari ya Shamu). Mtoto huyo alikuwa Mtume mtakatifu Muhammad (S.A.W). Jina aliloitwa mama yake mtoto huyo ni Bi Aaminah, binti wa Wahab bin Abdu-Manaf, ambaye alikuwa wa ukoo wa Zuhra, Baba yake naye aliitwa Abdullah, wa ukoo wa Banu Hashim. Baada ya siku kidogoAbdullah kumwoa BiAaminah, Abdullah alikwenda Shamu (Syria) katika msafara wa biashara. Alipokuwa akirejea nyumbani alishikwa na maradhi na akafa katika Madina;

wakati huo mji huu ulijulikana kwa jina la Yathrib. Kwa hivyo Muhammad (S.A.W) alizaliwa akiwa yatima asiye na baba. Kabla ya kuzaliwa Mtume mtakatifu (S.A.W), mama yake aliota kuwa kesha mzaa. Pia aliota kuwa lazima aitwe Muhammad maana yake asifiwaye. Aaminah aliona katika ndoto nyingine nuru kubwa inatoka katika mwili wake na kutapakaa katika nchi zote. Uchanga wa Muhammad (S.A.W) Watu wa Makka walikuwa wakiwapeleka watoto wao wachanga kwenda kulelewa na wanawake wa vijijini ambako hewa za huko zilikuwa nzuri zaidi kuliko hewa ya mjini.

1 Wanawake wa vitongoji kiasi cha maili thelathini au arobaini kutoka Maka walizoea kuja mjini na kuwachukua watoto wachanga waliozaliwa na kwenda nao kuwalea. Wanawake hawa walilipwa ujira wa kuwalea hawa watoto na wazazi wa watoto walipowarudisha wakati wa malezi ulipokwisha. Bi Aaminah alitaka mmoja wa mayaya hao kumlea Mtume Muhammad (S.A.W). Kila mmoja miongoni mwa wanawake hao aliposikia kuwa baba wa mtoto huyo amekufa alikataa kumlea, kwa kuogopa kuwa hatalipwa pesa za kutosha. Hawakujua kuwa yeye ndiye atakayekuwa Bwana wa Wafalme na Watawala. Njia za Mungu ni kinyume na njia zetu. MunguAlikwisha panga jinsiAaminah atakavyopata furaha na kuridhika, na jinsi Mtume Muhammad (S.A.W) atakavyolelewa kijijini. Miongoni mwa hao waliokuja Makka kuchukua watoto alikuwako mwanamke mmoja masikini, jina lake Halimah. Alibisha nyumba baada ya nyumba, akiuliza mtoto wa kulea lakini hapana wazazi waliotaka kumkabidhi mtoto wao kwa mwanamke masikini. Baada ya kukosa kumpata mtoto katika nyumba nyinginezo zote alikata shauri kumchukua huyo mtoto aliyekuwa hana baba, ili wanawake wengine wasije wakamchekelea kurejea nyumbani pasipo na mtoto aliyemchukua.

2 Utoto wa Muhammad (S.A.W). Muhammad (S.A.W) alipotimu miaka minne, Bi Halimah alimrejesha kwa mama yake, ambaye baada ya miaka miwili mingine alimpeleka kwa wazee wake katika mji wa Madina. Baada ya kukaa Madina kwa mwezi mmoja, walipokuwa wakirejea Makka pamoja na mtoto, Bi Aaminah alikufa wakiwa safarini. Kwa hiyo katika umri wa miaka sita Mtume Muhammad (S.A.W) aliachwa yatima asiye na baba wala mama. Mtu mmoja alimchukua na kumpeleka kwa babu yake Makka Bwana Abdul Mutwalib, lakini baada ya miaka miwili babu huyu naye alikufa, na hivyo Mtume Muhammad (S.A.W), akiwa na umri wa miaka minane alikwenda kuishi na baba yake mdogo aliyeitwa Abu Talib. Nyumba Mtume Muhammad (S.A.W) alimoishi alipokuwa mtoto hazikuwa za kitajiri, na watoto wengine hawakuwa na adabu nzuri. Wakati wa chakula ulipofika watoto walimzunguka mama yao, na kuitisha kwa sauti za juu kila chakula walichotaka. Kila mmoja alijaribu kupata chakula kingi kuliko wenzake. Lakini walipopiga kelele, Mtume Muhammad (S.A.W) alijikalia peke yake na kunyamaa, akimngoja mama yake mdogo (mke wa Bwana Abu Talib) ampe chakula, na alikula kwa furaha chakula cho chote alichopewa. Hata katika wakati huo wa umri mdogo, kila mtu aliyemjua Mtume Muhammad (S.A.W) aliona matendo yake yenye fikira;

下载(注:源文件不在本站服务器,都将跳转到源网站下载)
备用下载
发帖评论
相关话题
发布一个新话题