编辑: 黎文定 | 2016-09-04 |
na baba yake mdogo alimpenda sana hata alitaka Mtume Muhammad (S.A.W) awe naye wakati wote, mchana na usiku. Katika siku hizo walikuwa watu wachache katika bara Arabu walioweza kusoma ama kuandika, na kwa hivyo Mtume (S.A.W) alikuwa pasipo kujua mafunzo yoyote ya vitabu. Watu
3 walistaajabu kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alijua mambo mengi na alikuwa mtu mwenye busara sana ingawa hakuwa na ujuzi wa kusoma. Mtume Muhammad (S.A.W) alipokuwa na miaka kumi na miwili, baba yake mdogo alikuwa lazima aende Shamu kwa msafara wa biashara. Kijana huyu hakuweza - kustahimili upweke wa kumkosa baba yake mdogo kwa kutengana nae kwa muda mrefu hiyyo. KwahiyoAbu Talib alimchukua Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja nae safarini. Njiani walionana na mtu wa dini, Mkristo aliyeitwa Bahira, aliyeuona uso wa Mtume (S.A.W) na kuona alama za umaarufu wake wa siku zijazo. Mtunze mwana huyu . Bahira alimwambiaAbu Talibu. kwa sababu siku moja atapata kazi ya kumtumikia Mungu.
4 SURA YA PILI Umbo ........